Msemaji wa serikali Msigwa amlilia HansPope, aliniambia “ugonjwa unatesa sana huu”

Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa ameeleza jinsi alivyoguswa na msiba wa mdau mkubwa wa michezo nchini Tanzania, HansPope.


#Repost @gersonmsigwa with @make_repost
・・・
Nimeshtushwa sana na kifo cha Ndugu Zacharia HansPope. Tumepoteza mdau muhimu kwa soka la nchi yetu na mtu aliyetamani kuona Tanzania inakaa kwenye viwango vya kimataifa vya soka.

Poleni sana wanafamilia, uongozi wa @simbasctanzania wachezaji, wapenzi na wanachama wa @simbasctanzania wapenzi wa soka na wote walioguswa na msiba huu.

Mara ya mwisho niliwasiliana nae kwa kuchati nikimpa pole kwa maradhi yanayomkabili, alinijibu huku akiwa kwenye mashine ya oksijeni (mashine ya kumsaidia kupumua). Aliniambia “ugonjwa unatesa sana huu” na baadaye akasisitiza watu wachukue tahadhari.

Tumuombee apumzike mahali pema, tuwaombee wafiwa na tumuenzi kwa kuendeleza dhamira kubwa aliyekuwa nayo katika kuendeleza soka la Tanzania.

Mungu amweke mahali pema peponi, Amina.

Related Articles

Back to top button