Michezo

Msuva awachimba mkwara wanaomfukuzia kwa kutupia magoli ligi kuu Tanzania bara

Mshambuliaji wa Klabu ya Yanga, Simon Msuva wa Yanga amepiga mkwara mzito kwa wafungaji wenzake ambao anashindana nao kutupia magoli kwa msimu huu wa Ligi kuu Tanzania bara.
Msuva amesema hatishwi na kasi ya ufungaji ya wapinzani wake hao isipokuwa yeye anapambana kuhakikisha anafunga zaidi ili kuongeza mabao yake na kuhakikisha msimu huu ananyakua kiatu cha mfungaji bora wa msimu.
Kufunga ni kazi yao, hakuna haja ya kuwaogopa kwani na mimi nitapambana kuhakikisha nafunga kila ninapopata nafasi na si zaidi ya hapo, sina hofu na wafungaji wengine hawanitishi kabisa,“Alisema Msuva na kusisitiza kuwa
Mchezaji unatakiwa ujiamini kwa kile unachokifanya pia kumuomba Mungu kwa kila hatua mahali popote pale, sasa naamini nitafunga mabao mengi na kuwa mfungaji bora,Kwani katika maisha huwezi kupata kitu kirahisi pasipo kupambana, Naamini kila kitu kinawezekana hivyo nitamuomba Mungu anijaalie ili nisipatwe na maumivu”Alisema Simon Msuva kwenye mahojiano yake na Azam Tv.
Kwa sasa Simon Msuva ana magoli 12 akifungana na na Mshambuliaji wa Ruvu Shooting,Abdulrahman Mussa na kufuatiwa na Mbaraka Yusuph wa Kagera Sugar na Shiza Kichuya wa Simba wote wakiwa wamecheka na nyavu mara 11.
By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents