Mtangazaji wa Clouds FM Da’Huu asherehekea siku ya kuzaliwa kwa kutoa msaada Amana
Mtangazi wa Clouds FM kupitia kipindi cha Leo Tena, Husna Abdul aka Da’Huu akiambana wa wasanii wa muziki ameshereekea siku yake ya kuzaliwa weekend hii katika hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali.
Husna Abdul ambaye pia ameteuliwa kuwa BALOZI WA KUJITOLEA WA WATOTO katika hospitali hiyo, aliambatana na wafanyakazi wa Clouds FM, wasanii wa muziki, wadau na wasikilizaji wa kituo hicho cha redio.
Shilole na Da’huu wakiwa ndani ya hospitali ya Amana wodi ya watoto
Husna alitoa misaada ya vifaa tiba katika wodi ya wazazi katika hospitali hiyo ya Amana, kama sehemu ya maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa.
Kwa upande wake Husna Abdul alisema ameamua kufanya hivyo ili kuwasukuma watu wengine kukumbuka mahali ambapo walikozaliwa kuliko kupoteza pesa kufanya sherehe kubwa huku wakati huo huo kuna watu wanaojifungua kwa shida vifaa vya uzazi hakuna, hivyo kuwapa chagamoto wengine walione hilo.
Aidha kwa kupitia mwakilishi wa Mganga Mkuu wa hospitali ya Amana, Bi Getruda Masawe, alimshukuru Husna Abdul na Clouds kwa ujumla kwa kuwapatia misaada ya vifaa tiba hospitalini hapo na kuwaomba wengine waige mfano wa Balozi wa Watoto hospitalini hapo, Husna Abdul.
Mtangazaji wa Leo Tena ya Clouds Fm, Da’Huu
Shilole akizungumza na waandishi