Habari

Mtoto anayedaiwa kuuawa kwa kunyongwa kuzikwa leo (Video)

Mama mzazi wa marehemu Erickson Kimaro, Dkt. Digna Narcis Riwa akizungumzia tukio la mtoto wake mwenye umri wa miaka nane  ambaye anadaiwa kuuawa kwa kunyongwa  na msichana wa kazi nyumbani kwao Kimara Temboni Dar es Salaam.

Inadaiwa Mfanyakazi huyo wa ndani alifika kwenye nyumba hiyo ya mwajiri wake siku ya Jumamosi 28 Mei, 2022. Ameshinda siku ya Jumapili nyumbani na Jumatatu Mtoto alivyorudi kutoka shule mfanyakazi huyo akamnyonga mpaka kufariki dunia.

Digina anadai msichana huyi wa kazi walikuwa bado hawajamfahamu Vizuri  kwasababu ya kuwa busy tokea afike kwenye nyumba yao. Mama ni Daktari wa Moyo Hospitali ya Temeke, huku Baba akiwa ni Daktari wa Wanawake Hospitali ya Mloganzila.

Aidha Digna naendelea kueleza kuwa, msichana huyo wa kazi baada ya tukio hilo  alimpigia simu mama mtoto mida saa 11:30 jioni na kumweleza kuwa mtoto anaumwa na anashindwa kupumua vizuri. Baada ya Mama kufika akakuta mtoto ashakuwa wa baridi kichwani ila kiwiliwili cha moto, baada ya mtoto kukimbizwa Hospitali ya Mloganzila ilithibitika ameshafariki dunia.

Anasema msichana huyo wa huyo wa kazi alichukuliwa na Jeshi la Polisi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents