Habari

Mtwara: Kijana apandishwa kizimbani baada ya kumshawishi mwanaume mwenzake kumuoa

Kijana mmoja ambaye ni mkazi wa Manispaa ya Mtwara Sharifu Issah maarufu kama Zamda Salumu amefikishwa mahakamani kwa kosa la kufanya vitendo vya utovu wa kimaadili kwa kujifanya mwanamke na kumshawishi mwanaume mwenzake kufunga ndoa na kuishi pamoja kama mke na mume.

Akisoma kesi hiyo hakimu mkuu mkazi Richard Kabate amesema kosa hilo ni kinyume na kifungu cha 157 cha kanuni ya adhabu sura namba 16 ya sheria iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Kabate amedai kuwa mshtakiwa kati ya mwezi Machi mwaka huu na mwezi wa Juni akiwa katika vijiji vya Mkahala na Mpanyani halmashauri ya Nanyamba mkoa wa Mtwara kwa makusudi alijifanya mwanamke na kumshawishi Mustapha Saidi Nurdini kwa kumtongoza na kufunga nae ndoa isiyo halali.

Hata hivyo hakimu Kabete amesema kitendo hicho kinatoa tafsiri ya ukiukwaji mkubwa wa maadili kwa watu wa jinsia moja ya kiume kuishi kinyumba.

Mshtakiwa aliposomewa shtaka hilo na wakili wa serikali George Makasi amekana shitaka hilo na upelelezi wa kesi hiyo unaendelea mshtakiwa amerudishwa mahabusu na kesi hiyo itatajwa mahakamani hapo Septemba 28, 2017.

Souurce: ITV

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents