Burudani

Mume wa Wendy Williams apitiwa na ‘shetani’

Kauli ya Diamond Platnumz ya kupitiwa na shetani kwa kutembea na Hamisa Mobetto, imeanza kuwa ni ya kweli kwani mastaa kadhaa wamekuwa wkiripotiwa kuchepuka katika familia zao. Mume wa mtangazaji machachari Wendy Williams, Kevin Hunter amekuwa moja ya watu waliopitiwa na shetani kwa kuchepuka katika ndao yake.


Kwa mujibu wa  ripoti ya Daily Mail umebaini kuwa Kevin amekuwa na mahusinao ya kimapenzi na Sharina Hudson mwenye miaka 32, kwa muda mrefu ambapo wamefanikiwa kupata picha pamoja na video za wawili hao.

Ripoti hiyo  imeonyesha kuwa Kevin amekuwa akijigawa katika maisha ya ndoa yake  kwa kuwepo New Jersey, alipo mkwe na kisha kutembelea Morristown alipo kimada wake Hudson.

 

Kevin Hunter na Sharina Hudson

Hii siyo mara ya kwanza kwa tukio hilo ambapo mwaka 2001, Wendy alimkuta mumewe akimsaliti ikiwa ni muda mchache tangu kujifungua  mtoto wao lakini baadaye akasema tukio hilo limewafanya wawe imara.

Siku chache zilizopita kabla ya ripoti hii wawili hao walikuwa katika fukwe za Barbados, wakifurahia mahusiano yao lakini baada ya ripoti hii kutoka mahusiano yao yameanza kulegalega. Kwa upande wa  Hudson  yeye amevaa pete aliyopewa na Kevin akiamini ndoa yake na Wendy itavunjika ili aweze kupata nafasi ya mama mjengo.

Kevin na Wendy wameoana kwa takribani miaka 20, na wanamtoto aitwaye Kevin Jr aliyezaliwa mwka 2000. Kevin amekuwa akifanya kazi ya production na kusimamika kipindi cha TV cha mkewe.

 

Kevin Hunter na Sharina Hudson

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents