Habari

Muuzaji wa duka linalodaiwa kumwonesha ubaguzi wa rangi Oprah Winfrey nchini Switzerland akanusha kumbagua!

Muuzaji wa duka la urembo la Trois Pomme huko Zurich aliyedaiwa kukataa kumhudumia bilionea wa talkshow Oprah Winfrey kwa kudhani hataweza kumudu gharama kwasababu ni mtu mweusi, ameibuka na kukanusha kwa kusema Oprah ni muongo sababu hakumbagua.

Oprah-

Akizungumza na gazeti la Jumapili SonntagsBlick la Switzerland , muuzaji wa duka hilo muitaliano alisema:
“Mimi sikuwa na uhakika nini cha kumpatia alipokuja mchana wa Jumamosi Julai 20, hivyo nilimuonesha baadhi ya mikoba iliyopo kutoka Jennifer Aniston. Nilimuelezea mikoba huja katika ukubwa tofauti na material tofauti kama ambavyo huwa nafanya”.

Oprah-4
Mkoba mweusi wa kulia ndiyo Oprah aliotaka kuuona

Muuzaji huyo aliendelea kueleza “Aliangalia katika fremu ya nyuma yangu na kwa mbali kulikuwa na Swiss franc crocodile leather bag ya 35,000. Mimi nikamuelezea kuwa mkoba huo ni sawa na ule niliokuwa nao mkononi lakini una gharama kubwa zaidi, na pia nikamwambia ninaweza kumuonesha mikoba mingine inayofanana na huo. Sio kweli kabisa kwamba nilikataa kumuonesha mkoba alioutaka kwasababu za kibaguzi , na nilimuuliza pia kama anahitaji kuutazama mkoba huo”.

Oprah duka
Hili ndiyo duka aliloingia Oprah kwa lengo la kununua mkoba

Muuzaji huyo alisema baada ya hapo Oprah aliendelea kuangalia kidogo dukani hapo na kisha kuamua kuondoka bila kusema kitu chochote.

Mwezi uliopita (July) Oprah alienda Zurich, Switzerland kuhudhuria harusi ya mwimbaji Tiner Turner.
Kwa mujibu wa Oprah alipokuwa Zurich alienda kwenye duka la urembo Trois Pomme ili kutafuta mkoba wa kuendana na vazi lake kwaajili ya harusi, na kuona mkoba unaouzwa $38,000 sawa na zaidi ya shilingi milioni 60, na alipohitaji muuzaji ampe mkoba auone alimjibu ni wa gharama kubwa hawezi kuumudu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents