Mvua yaleta balaa!
Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wamekumbwa na mvua kubwa ambayo imeonekana kuleta athari kwa kiasi kikubwa sana na kupelekea kusimama kwa shughuli nyingi za kijamii na kuharibu makazi na mali mbali mbali za wananchi.

Mvua hiyo ambayo ilianza majira ya mchana wa saa 6 mpaka kufikia nyakati za jioni, wakazi wengi sana walionekana kwa wingi kwenye vituo vya daladala wakisubiri usafiri ambao ulikuwa ni wa tabu sana kutokana na msongamano karibu njia zote za jiji. Hali hii imesababisha baadhi ya raia kuamua kutembea kwa miguu wakielekea majumbani kwao.
Mvua ya leo pia imesababisha uharibifu wa hali ya juu katika maeneo mbali mbali ya jiji, na kwenye jamii na makazi kwa ujumla.
Mdau wa bongo5 ametuletea picha hizi kuonesha uharibifu uliowakumba wafanyakazi wa ofisi moja mitaa ya uwanja wa ndege: