Habari

Mwanaume akamatwa kwa kumiliki kichwa na sehemu za siri za kiume

Mwanaume mmoja amekamatwa katika jimbo la kati la Sofala nchini Msumbiji kwa kumiliki kichwa na sehemu za siri za mwanaume, polisi wamesema.

Watoto waligundua sehemu za miili hiyo kwenye mfuko wa plastiki katika wilaya ya Nhamatanda na kutoa taarifa kwa mamlaka, alisema Dércio Chacate, msemaji wa kamandi ya polisi ya Sofala.

Uchunguzi ulipelekea kukamatwa kwa mtu huyo ambaye alikiri kumuua mtu kisha kumkata kichwa na sehemu zake za siri ili aweze kuziuza, alisema.

Mshukiwa alikiri kuua na kukata vichwa vya watu wengine watatu, Bw Chacate alisema.

Uchunguzi ulikuwa ukiendelea ili kuwakamata wanaodaiwa kuwa wapangaji na wanunuzi.

Viungo vya mwili hutumiwa na baadhi ya wanaoitwa madaktari wa jadi kutengeneza dawa, ambazo kwa uwongo wanadai zinaweza kutibu magonjwa, kuondoa dalili mbaya na kuboresha maisha ya watu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents