Habari

Mwandishi Soyinka atimiza ahadi yake ya kuhama Marekani kabla hata ya kuapishwa kwa Donald Trump

Mwandishi maarufu duniani mwenye asili ya nchini Nigeria anayeishi Marekani, Wole Soyinka ametiza ahadi yake ya kuiharibu kadi yake inayompa nafasi ya kuishi nchini humo (Green Card) kabla hata Donald Trump hajaapishwa kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.
_92792353_bd877e2a-18d0-4695-b7cb-73022a55412d

Mwezi uliopita mshindi huyo wa tuzo la fasihi alisema kuwa angeirarua green card, ambayo humpa mtu kibali cha kuishi nchini Marekanai ikiwa Dionald Trump angechaguliwa kuwa rais wa Marekani.

Aliliambia shirika la AFP mjini Johannesburg kuwa kutokana na vile Trump ameshinda, basi ametekeleza alichokisema

“Tayari nishafanya, nimetoka Marekani , nimefanya kile nilisema ningekifanya, nilitupa green card yangu , nimerudi penye ninastahili kuwa,” alisema Soyinka.

Hata hivyo Soyinka hawashauri watu wengine kufuata mkondo huo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents