Habari

Mwili wa Ndesamburo waanza kupelekwa uwanja wa Majengo

Mwili wa Mbunge wa zamani wa Moshi mjini, Philemon Ndesamburo tayari umepakiwa katika gari maalumu kwa ajili ya kupelekwa katika uwanja wa Majengo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

Mwili huo ulikuwa unehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya KCMC tangu alipofariki dunia ghafla Jumatatu iliyopita baada ya kuugua.

Msafara huo utapita barabara ya KCMC hadi mzunguko wa magari wa YMCA na baadae kupita barabara kuu ya Moshi-Dar hadi Majengo.

Chanzo: Mwananchi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents