Bongo Movie

Mzee Zahil Ally Zorro kuigiza mkuu wa upelelezi kwenye filamu ya Hashim Kambi ‘Fisadais’

Mwanamuziki mkongwe nchini, Zahil Ally Zorro ambaye ni baba yao mzazi na wasanii Banana na Maunda, ataonekana kwenye filamu mpya iitwayo Fisadais. Katika filamu hiyo, Mzee Zahil ameigiza kama mkurugenzi wa kitengo maalum cha upelelezi.

Banana Zorro taking a pose

Hiyo ni filamu ya pili iliyoongozwa na muigizaji na muongozaji wa filamu, Hashim Kambi.

“FISADAIS ni zaidi ya ufisadi na imechezwa na mimi mwenyewe na mke wangu akiwa mama Hidaya Njaidi pia yumo kijana machachali Mbotto na mwanangu amekuwa Mainda bila kumkosa mzee Jengua na kwa mara ya kwanza nimemshirikisha Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa Rhumba mzee ZAHIL ALLY ZORRO akicheza kama mkurugenzi wa kitengo maalum cha upelelezi,” ameandika Hashim kwenye ukurasa wake wa Facebook.

“Sikumuacha binti aliyecheza vizuuri katika filamu yangu ya Binti yangu aitwaye Diana Exavery. Nategemea movie hii itatoka mnamo mwisho wa mwezi JUNE mwaka huu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents