Burudani

Ngoma ya ‘Bodak Yellow’ ya Cardi B yavunja rekodi Billboard

Rapper  Cardi B amekuwa wa kwanza  kwa takribani  miaka 19 kwa kutinga nafasi ya kwanza  katika chati za muziki za Billboard Hot 100 bila kollabo.

Cardi B ameweka rekodi hiyo kupitia ngoma yake ya ‘Bodak Yellow’ mwaka 1998 Lauryn Hill ndiyo alikuwa ameshika nafasi hiyo kupitia ngoma ya Doo Wop (That Thing).

Mrembo mwenye asili ya Latini ambaye amekuwa tishio kwa marapper wa kike kama Nick Minaj ameweka rekodi hiyo Septemba 25, 2017 kwenye chati hizo mama za muziki Marekani na kwa kuitoa ngoma ‘Look what you made me do’ ya mwanadada Taylor Swift.

Cardi B alikuwa akishika namba mbili kwa muda mrefu kabla ya kuongoza na pia ni msanii wa Latina kuongoza chati hiyo toka mwaka 2006 ambapo Shakira  aliwakilisha kupitia ‘Hips Don’t Lie’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents