Burudani

Gurumo akabidhiwa Milioni 2

Twanga_ngurumo_muhidini

 

African Stars Entertainment imemkabidhi Mwanamuziki mkongwe Nchini Muhidin Gurumo wa Msondo Ngoma Music Band kiasi cha shilingi Milioni mbili za kitanzania zilizokusanywa kutokana na onyesho lililofanyika Jumamosi iliyopita katika ukumbi wa Mango Garden.

ASET Iliandaa onyesho hilo kwa lengo la kutafuta fedha ili kumchangia Mwanamuziki huyo kwa ajili ya kugharamia matibabu anayoendelea kuyapata pamoja na kujikimu. Fedha hizo zilikabidhiwa kwa Mzee Ngurumo na Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka akiongozana na meneja wa Msondo Ngoma Music Band Said Kibiriti na Meneja wa ASET Hassan Rehani nyumbani kwake Mzee Ngurumo Mabibo Makuburi.

Mara baada ya kukabidhiwa Mzee Ngurumo alitoa shukrani nyingi kwa Asha Baraka kwa kufanikisha mpaka yeye kupata kiasi hicho cha fedha ikizingatiwa kwa sasa yeye kutokana na maradhi hawezi kufanya kazi kwa sasa.

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents