Habari

Nicki Minaj asema hakumdiss Iggy Azalea kwenye tuzo za BET, ‘The media puts words in my mouth’

Baada ya maswali mengi kuhusu kama Nicki Minaj kweli alimdiss rapper mwenzake wa kike Iggy Azalea kwenye Tuzo za BET weekend iliyopita, Minaj ameibuka na kusafisha anga kwa kutoa ufafanuzi wa kile alichokiongea baada ya kushinda tuzo ya ‘Best Female Hip Hop Artist’.

nicki-minaj-bet-awards

Nicki ameamua kuzungumzia swala hilo kupitia twitter na kusema vyombo vya habari vinamuwekea maneno kinywani, ila alichomaanisha kwenye hotuba yake ni kuwahamasisha wanawake kuandika wenyewe mawazo na mitazamo yao.

Iggy Azalea Visits MTV's "Hip Hop POV"
Iggy Azalea

Pia akaongeza kuwa amewahi kumpongeza Iggy kwa mafanikio ya wimbo wake ‘Fancy’ hadharani.

“Vyombo vya habari huwa vinaniwekea maneno kinywani siku zote na hakuna tofauti, nitaendelea kushikilia msimamo wa wanawake kujiandikia kwasababu nina imani juu yetu, nina amini tuna uwezo mkubwa wa kuandika mawazo na mitazamo yetu kama wafanyavyo wanaume, nimekuwa nikilisema hili kwa miaka mitano. Nilimpenda Lauryn Hill kwasababu nilijua alikuwa anaandika mwenyewe.” Aliandika.

nicki tweets
n2

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents