Habari

Nilipewa ‘si zaidi ya dakika mbili’ kujiandaa kutoroka Ikulu – Ashraf Ghani

Rais wa zamani wa Afghanistan, Ashraf Ghani amesema alipewa ‘si zaidi ya dakika mbili’ kujiandaa kutoroka Ikulu Kabul mwezi Agosti wakati kundi la Taliban wakiuteka mji mkuu wa nchi hiyo.

Ghani amekiambia chombo cha habari cha BBC’s Radio 4 kwamba Mshauri wake wa Usalama wa Taifa alimweleza kuwa lazima aondoke na kusema kuwa ilikuwa ghafla na kuongeza kuwa walipoondoka tu ikawa wazi wanaoondoka Afghanistan.

“Asubuhi ya siku hiyo, sikuwa na fahamu kwamba kufikia jioni, alasiri nitaondoka,” Ghani alisimulia wakati wa mahojiano na Mkuu wa zamani wa Majeshi ya Uingereza Jenerali Nick Carter, yaliyotangazwa siku ya Alhamisi. Carter alikuwa mgeni akihariri toleo hilo la kipindi cha redio cha BBC.

Ghani amekanusha kuwa kulikuwa na mazungumzo yaliyokuwa yanaendelea wakati huo ya makubaliano ya kuwachia madaraka kwa amani, kama walivyodai maafisa wa zamani wa Afghanistan na Marekani.

Source: CNN

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents