Burudani

Njia rahisi ya kuishi mjini, kwa mujibu Diamond

Msanii Diamond Platnumz ametoa somo la namna watu wanavyotakiwa kuishi mjini.

Muimbaji huyo wa ngoma ‘Waka’ amesema ingawa kila mmoja anauelewa wake ila ni muhimu kutoa nafasi kwa wengine kuongeze kitu kwa kile ambacho unakijua.

“Unajua mjini sio kuishi kwa kujua ni, ni namna unavyoishi na watu tu, inawezekana mimi ninajua kitu kuishia hapa lakini kumbe wewe unajua kuanzia nilipoishia mimi na kwenda mbele,” Diamond amesema hayo katika Interview na Bagdad.

“Kama nina mazungumzo mazuri na wewe huwezi kuniacha mimi niangaike nisiendelee utanisaidia ili nisogee, kwa hiyo si kujua ni kuangalia njia gani unazitumia na unaishije na watu, it’s all about techniques,” amesisitiza.

Diamond kwa mwaka huu hajatoa ngoma mpya ila kichosubiriwa kwa hamu kutoka kwake muda huu ni ujio wa albamu yake mpya ‘A Boy From Tandale’ na vyombo vyake vya habari (Wasafi TV/Radio).

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents