Habari

NMB yatoa msaada wa vifaa vya hospitali Tarime vijijini, Ushetu, Mikumi na Madawati Ndanda

Benki ya NMB imetoa msaada wa vifaa vya hospitali; vitanda, magodoro na mashuka vyenye thamani ya shilingi milioni kumi na tano kwa hospitali za halmashauri za wilaya za Tarime vijijini(Mara), Ushetu katika wilaya ya Kahama (Shinyanga) na Mikumi- wilaya ya Kilomero (Morogoro).

Vifaa hivyo vimekabidhiwa wakati Benki hiyo ikizindua huduma mpya tatu za kibabe katika maeneo mbali mbali nchini; Namba ya WhatsApp 0747333444, njia ya digitali ya kutoa maoni kwa mfumo wa kuscan QR pamoja na mfumo wa kurudisha token za umeme (token retrieval) wakati wakiadhimisha wiki ya huduma kwa wateja.

Hospitali mpya ya Halmashauri ya wilaya ya Tarime iliyopo Nyamwanga ilikabidhiwa vitanda saba vikiwemo viwili vya kujifungulia na magodoro. Akipokea msaada huo Katibu Tawala wa wilaya ya Tarime, John Marwa alisema msaada huo utaboresha huduma za matibabu katika hospitali hiyo ambayo inahudumia zaidi ya watu 300,000 wakiwemo wamama wajawazito.

Mkuu wa Mauzo – Idara ya Hazina ya Benki ya NMB, Jeremiah Lyimo (wapili kutoka kushoto) akikabidhi msaada wa vitanda saba vikiwemo viwili vya kujifungulia na magodoro kwaKatibu Tawala wa Wilaya ya Tarime – John Marwa, watatu kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Apoo Castro Tindwa, Meneja wa NMB Tawi la Nyamongo, Erick Manyama(mwenye miwani) pamoja na Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa, Baraka Ladislaus.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents