Habari
Nyota wa filamu ya Rocky, Sylvester Stallone ‘Rambo’ aondolewa mashtaka ya ubakaji
Nyota wa filamu ya Rocky, Sylvester Stallone ‘Rambo’ ameondolewa mashtaka ya kumbaka mwanamke mmoja ambaye awali alikuwa na uhusiano wa kimapenzi naye.
Dada huyo ambaye ndiye mwathirika mkuu wa tukio hilo alimshitaki Stallone kwa kumbaka mnamo mwaka 1987 na 1990 na kutoa mashahidi wake ambapo hata hivyo hawakutoa ushirikiano wa kutosha kwenye upelelezi wa kesi hiyo.
Madai hayo yalifunguliwa na mwanamke huyo mwezi Novemba mwaka 2017 na marakadhaa Stallone amekuwa akikanusha mashtaka hayo.
Mwendesha mashtaka wa jimbo la California amemuondolea mashtaka baada ya kukosa ushahidi aidha muigizaji huyo anakila sababu ya kutabasamu baada ya mkuu wa sheria wa Los Angeles kusema madai ya mwanamke huyo ya mwaka wa 2017 hayakuwa ya kweli.