Burudani

Nyota za Rama Dee kwa Diamond Platnumz

Mkali wa muziki wa RnB Bongo, Rama Dee amempongeza Diamond Platnumz kwa namna anavyopigania sanaa yake.

Muimbaji huyo amesema hatua aliyofikia Diamond inampa furaha. Kupitia Instagram yake ameandika;

Msanii wa kwanza Tanzania kupata freedom, nasikia furaha sana kuona msanii anaweza kuongea Kama msanii sio Mtumwa wa fikra…. Big up Nasibu, Mungu akuongezee maisha!

Utakumbuka leo June 19, 2018 Diamond alikuwa na mkutano na waandishi wa habari na kuzungumza mambo kadhaa kuhusu sanaa na upande wa Wasafi Media,

Kikubwa kilichogonga vichwa vya habari ni ujio wa Wasafi Festival ambapo ameeleza itapita kwenye mikoa mbali mbali na kujumuisha wasanii hata wale walio nje ya WCB na kusisitiza wote watalipwa vizuri.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents