Uncategorized

Ole Gunnar Solskjaer abadili gia angani ‘Sina ndoto za kuwa top four, tupo hapa kwaajili ya kutwaa ubingwa’

Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amesisitiza kuwa kamwe hawezi kurizika kwakuwa nafasi ya nne ya ligi kuu nchini Uingereza na kusema kuwa kushinda mataji ndiyo lengo pekee ndani ya Old Trafford.

Wakati mashabiki wa United wakitamani kuiyona klabu hiyo inatinga nafasi ya nne ikitoka ya sita ambayo ipo kwa sasa hivi, huku kocha wa Tottenham Hotspu, Mauricio Pochettino akiamini kuwa timu hiyo inahaha ili kuingia kwenye nafasi hizo za juu ili kupata kibali cha kushiriki michuano ya Champions League, Solskjaer amesema hiyo siyo ndoto yake bali lengo lake ni kushinda taji la ligi.

Akionekana kama kumjibu Mauricio Pochettino, kocha huyo wa United amesema ‘’Hiyo siyo ndoto yangu kuwa kwenye nafasi nne za juu, sisi kama Manchester United, siku zote lengo letu kuu ni kushinda taji la ligi.’’

‘’Hatutoweza kufanya hivyo mwaka huu lakini tutaendelea kupambania hilo kwasababu tumerudi kwenye ubora.’’

‘’Tulishashinda Champions League na hata FA Cup, hivyo hatuwezi kusema nafasi nne za juu kwenye msimamo wa ligi ndiyo lengo, ni lazima tuangalie mbali zaidi, Je ni kwa kiasi gani tunaweza kutwaa kitu chohcote mwaka huu ?.’’

‘’Ninakwenda kwenye kila mchezo kama kocha wa United huku nikifikiria namna ya kushinda mchezo. Bado tupo kwenye michuano ya FA Cup na tunahitaji kujaribu kuona kama tutashinda taji hilo.’’

‘’Sipo hapa kwaajili ya kujibu alichozungumza Pochettino lakini nipo hapa kuhusiana na kushinda mataji, bila shaka ukitwaa mataji ndiyo jambo bora kwa kila mmoja.’’

Solskjaer atakuwa katika uwanja wake nyumbani Old Trafford usiku wa leo akiwakaribisha Burnley mchezo wa Primier League.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents