One Billion Rising yaadhimisha Valentine’s Day na tamasha la kupinga ukatili dhidi ya wanawake


Wakazi wa jiji la Dar es salaam,jana alasiri walijiunga na wanaharakati duniani kote katika kuadhimisha kampeni ya One billion Rising katika harakati za uhamasishaji wa kimataifa wa kukomesha ukatili dhidi ya wanawake na wasichana.

Vuguvugu la One billion Rising lilianza kama wito wa kuchukua hatua kutokana na takwimu ya kushtua, kwamba mwanamke 1 kati ya 3 duniani atapigwa au kubakwa wakati wa uhai wake. Kwa kuwa idadi ya watu duniani imefikia bilioni 7, hii inamaanisha zaidi ya Wanawake na wasichana bilioni 1 wana uwezekano wa kuwa wamepata madhara ya aina hiyo.

Nancy Sumari na Faraja Kota wakisoma shairi
Nancy Sumari na Faraja Kota wakisoma shairi

Katika kuadhimisha Valentine’s Day wanaharakati wa mradi wa Endeanger Health Champion wakishirikiana na taasisi ya umoja wa mataifa nchini UNFPA kitengo cha programu ya afya waliandaa tamasha la elimu la kukomesha ubakaji lililopewa jina la ” Tuamke Dar”.

Tamasha hilo lilijumuisha pia wanaharakati,waandishi,wanafalsafa, watu mashuhuri,na wanawake na wanaume duniani kote kuonyesha hasira zao, kudai mabadiliko, kusoma, kucheza na kuamka ili kupingana na mateso ya uonevu wayapatayo wanawake,hatimaye kukomeshwa kwa ukatili dhidi yao.

Kampeni hiyo inategemewa kuchochea kubadili dunia,kuhamasisha wanawake na wanaume kucheza ngoma katika kila nchi.

Esther Majani afisa Endeanger Health Champion akifurahia jambo na girl guides
Esther Majani afisa Endeanger Health Champion akifurahia jambo na girl guides

Akisoma risala kutoka kwa katibu mkuu wa umoja wa mataifa, afisa programu za kijinsia katika ofisi ya UNFPA Anna Holmstrom alisema ujumbe ulioletwa kwa wakazi wa Dar es Salaam mwaka huu ni kupinga, kukataa na kuacha vitendo vyote vya unyanyasaji wa kijinsia hasa hasa ubakaji kwa wanawake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents