Burudani

Navio: Goldie believed in a bigger Africa that went beyond her own borders

Navio

Kila mtu aliyekuwa akimfahamu Goldie amehuzunishwa na kifo chake cha ghafla lakini wapo walioumia zaidi ambao ni ndugu, jamaa na marafiki zake wa karibu. Kwa Afrika Mashariki kuna watu watatu walioumizwa zaidi na kifo chake.

DETAILS: NI KWELI GOLDIE AMEFARIKI DUNIA, LABEL YAKE YATOA TAARIFA RASMI!

Wa kwanza bila shaka ni Prezzo ambaye ndoto zao za kuja kuwa mtu na mke wake zilikuwa zimeanza kutumia. Ni Jumanne hii tu kwenye kipindi cha Churchill Live, Prezzo aliweka wazi uhusiano wao baada ya kuwepo uvumi wa muda mrefu. Kwenye kipindi hicho, Prezzo alidai kuwa ameanza kukusanya mahari kwaajili ya kupeleka kwa wazazi wa staa huyo nchini Nigeria na kwamba lazima angemuoa.

prezzo 22

Jana pia alidaiwa kukwea pipa hadi nchini Nigeria kuungana na kipenzi chake kwenye siku ya wapendanao iliyogeuka kuwa siku mbaya katika maisha yake kwa kumpoteza mrembo huyo. Bado Prezzo hajasema lolote lakini ni wazi kifo cha Goldie ni pigo kubwa kwake.

Wa pili ni Navio wa Uganda. Wawili hao walikuwa wameshafanya wimbo pamoja uitwao Kamili na video itatoka hivi karibuni.

Navio goldie

Navio anasema alimchukulia Goldie kama dada yake mdogo na tangu kusambaa kwa habari hizo amekuwa akiandika mara kwa mara jinsi alivyoumizwa na kifo hicho.

“My little sister has passed away. Goldie Harvey honourably Represented Nigeria in the Big Brother House, and was on the fast track to changing the Industry. She believed in a bigger Africa, that went beyond her own borders. Goldie Harvey was an inspiration to me. And will always be my little sis. Rest in Peace Babe,” ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.

“@GoldieHarvey We miss you already. You were about to change Africa in ways we can’t even understand now. You are my sister, always,” ametweet.

Wa tatu ni Ambwene Yesaya aka AY ambaye Goldie alimshirikisha kwenye wimbo wake Skibobo.

Ay+na+Goldie1

Bado AY hajasema lolote huenda bado anatafakari habari hizo za kuhuzunisha.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents