Burudani

P-Funk aelezea Bongo Fleva ilivyotoka kwenye kuitwa muziki wa kihuni hadi kuwa wenye heshima

Producer wa Bongo Records, P-Funk Majani amesema muziki wa Bongo Flava sasa umegeuka kuwa miongoni mwa vitu vinavyoheshimika zaidi nchini.

_MG_2238

Akiongea na kituo cha runinga cha Azam Two kwenye hafla ya wasanii kumuaga Rais Jakaya Kikwete, Majani alisema zamani heshima haikuwepo kabisa.

“Sasa hivi kila mtu anaitambua Bongo Flava na anaikubali,” anasema Majani.

“Hata pia viongozi wetu zamani walikuwa kidogo wakisikia kuhusu muziki wanaona kitu cha uhuni au nini. Imeonekana ni biashara, makampuni pia yamekuja yamejitokeza yanawekeza kwenye muziki,” ameongeza.

“Wasanii wenyewe wameongezeka. Pia tumeweza kupanua mipaka yetu, sasa hivi tunasikika Afrika nzima so haya ni mafanikio makubwa. Teknolojia pia imesaidia lakini kwa ufupi watu wameanza kusupport muziki wao, kuupenda na kuuthamini.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents