Michezo

Pablo Franco: Sisi ndiyo Mabingwa wa michuno hii 

Kocha wa Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Azam Sports Federation na Mapinduzi Cup Simba SC, Pablo Franco amesema kuwa watahakikisha wanafanikiwa kulitetea taji lao la michuano ya ASFC kwa kuwafunga Ruvu Shooting hapo kesho.

”Sisi ndiyo Mabingwa wa michuano hii na malengo yetu ni kuhakikisha tunavuka hatua na kwenda robo fainali na hatimaye tulitetee kombe letu.” – Kocha wa klabu ya Simba Pablo
Simba itashuka katika uwanja wa Benjamin Mkapa hapo kesho siku ya  Jumatano ya Februari 16, 2022 kuwakabili vijana wa Masau Bwire, Ruvu Shooting mchezo wa raundi ya 16 Bora.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents