Habari

PARIS: Kijana mwenye hasira avamia kituo kikubwa cha polisi nchini Ufaransa na kuua askari wanne kwa kisu

Kijana mmoja ambaye hajafahamika hadi hivi sasa, Amevamia kituo cha polisi Jijini Paris nchini Ufaransa na kuwashambulia kwa kisu askari waliokuwepo zamu katika kituo hicho.

Polisi mjini Paris wamesema kuwa mtu huyo aliingia katika kituo cha kati cha  île de la Cité akiwa na kisu na kisha kuanza kuwashambulia maaskari hao, Ambapo walilazimika kujihami kwa kumpiga risasi.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa,  Christophe Castaner amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amesema mpaka sasa Askari wanne wamefariki dunia kwenye tukio hilo.

Hata hivyo, Bado haijaelezwa nini chanzo cha tukio hilo, Ingawaje imeelezwa kuwa mtekelezaji wa tukio hilo aliingia katika kanisa la Kikatoliki la Notre Dame lililo karibu na kituo hicho cha polisi kabla ya kupata upenyo wa kuingia kituoni hapo.

Tukio hilo limetokea majira ya saa 7;00 mchana wa leo Oktoba 3, 2019 na imeelezwa kuwa hali ya usalama kwasasa imeimarishwa.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents