Michezo
Picha: Bastian Schweinsteiger afunga ndoa na Ana Ivanovic
Bastian Schweinsteiger na mchumba wake, mchezaji wa tennis, Ana Ivanovic wamefunga ndoa.
Schweinsteiger ambaye ni mchezaji wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Ujerumani, amefanikiwa kufunga ndoa Jumanne hii kwenye ukumbi wa Venice City Hall na mchumba wake huyo raia wa Serbia.
Sherehe hiyo imehudhuriwa na ndugu pamoja na watu wa karibu wa familia hiyo akiwemo kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joachim Low, Thomas Muller, Kerber na Andy Murray.
Wawili hao walianza mahusiano mwaka 2014 baada ya Schweinsteiger kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Sarah Brandner waliodumu kwenye mahusiano kwa takriban miaka saba.