Burudani

Picha hizi zinathibitisha kuwa Drake na Serena Williams ni wapenzi

Mtandao wa TMZ umepata picha zinazothibitisha kuwa rapper Drake na mchezaji tennis mahiri, Serena Williams ni wapenzi.

0824-drake-serena-williams-launch3-3

Wawili hao walionekana pamoja kwenye mgahawa wa huko Cincinnati.
Masaa machache baada ya Serena kushiriki na kushinda kwenye mashindano ya WTA ambapo Drake alimshuhudia na baadaye walijumuika pamoja kwenye mgahawa Sotto.

0824-subasset-drake-tennis-open-instagram-3

Wawili hao walikuwa na chumba binafsi nyuma ya mgahawa huo ambapo mara nyingi walionekana kushikana na kupiga busu. Watu waliokuwepo ndani ya mgahawa huo wameiambia TMZ kuwa watu wengine 6 waliungana nao.

Kumekupo na tetesi za wawili hao kuwa wapenzi kwa miezi sasa tangu Drake alipoonekana akimshangilia Serena kwenye mashindano ya Wimbledon.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents