Burudani

Picha: Iggy Azalea azama kwenye penzi jipya la mtayarishaji wa muziki

Baada ya kuyeyuka kwa penzi la Iggy Azalea na French Montana, sasa mrembo huyo amehusishwa kuingia katika penzi jipya na mtayarishaji wa muziki nchini Marekani.

Jumapili hii Iggy alionekana katika fukwe za eneo la Cabo San Lucas akila bata katika boti binafsi akiwa na Ljay Currie ambaye ndio anadaiwa kuwa mpenzi wake kwa sasa pamoja na marafiki zao wengine wa karibu. Ljay ni mtayarishaji wa muziki ambaye aliwahi kufanya kazi na Chris Brown.

Wakati huo huo Agosti mwaka jana Iggy na French walionekana katika fukwe hizo za nchini Mexico wakila bata pamoja. Tazama picha zaidi za Iggy na Ljay hapa chini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents