Bongo Movie

Picha: Msimu wa pili wa tamthilia ya ‘Siri ya Mtungi’ wazinduliwa Dar

Msimu wa pili wa Tamthilia ya ‘Siri ya Mtungi’, leo umezinduliwa jijini Dar es Salaam ambapo utaanza kuoneshwa rasmi Jumapili, December 7 katika vituo mbalimbali vya runinga.

Mtayarishaji wa tamthiria ya Siri ya Mtungi Louise Kamin akizungumza na waandishi wa habari
Mtayarishaji wa tamthilia ya Siri ya Mtungi, Louise Kamin akizungumza na waandishi wa habari

Akizungumza na waandishi wa habari ndani ya ukumbi wa Hadees Fast Food uliopo Posta jijini Dar es Salaam, mtayarishaji wa tamthilia ya ‘Siri ya Mtungi’, Louise Kamin alisema msimu huu ndo utakuwa wa mwisho baada ya siri zote kujulikana.

“Tutazindua Siri ya Mtungi msimu wa pili Jumapili hii inayokuja tarehe saba ndani ya TBC kuanzia saa kumi na mbili na nusu jioni,” alisema.

“Msimu wa kwanza wa tamthilia ulikuwa kivutio cha watu wengi wa upande wa Afrika ya Mashariki na kuacha maswali kibao na hii tutokana na tamthilia kubeba vionjo halisi vya maisha katika jamii na hasa kwa wakazi wa mkoa wa Pwani wa Tanzania na hapo ikaanza kupokelewa vizuri na kutambuliwa hasa kwenye maonyesho maarufu ya tuzo za Africa Magic Viewers’ Choice Awards mwaka huu 2014 na kupata uteuzi kwenye makundi saba ya ubora, kipindi cha television, maker-up, mavazi, mwelekeo wa sanaa, maandalizi ya sauti, Uigizaji na kipindi cha lugha yake ya Kiswahili. Kwahiyo ningependa kusema natoboa siri kwamba msimu huu wa Siri ya Mtungi utakuwa wa mwisho na inasikitisha sana lakini siri imefichuka. Nadhani tamthilia ya Siri ya Mtungi imefika mwisho wake,” aliongeza.

Director wa Siri ya Mtungi Karabani akizungumza
Director wa Siri ya Mtungi, Karabani akizungumza

Karabani, Cheche na Louse
Karabani, Cheche na Louise

Mwigizaji wa Siri ya Mtungi Cheche
Mwigizaji wa Siri ya Mtungi, Cheche

Producer & Director Jordan Riber kutoka Hollywood
Producer&Director Jordan Riber kutoka Hollywood

Waandishi wa habari
Waandishi wa habari

Waandishi
Waandishi

Wanahabari (2)
Wanahabari

IMG_7308

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents