Promotion

Vodacom yaja na huduma ya Vinjari na M-Pesa

Katika kuzidi kurahisisha huduma za malipo wakati tukielekea msimu wa sikukuu za Krismas na Mwaka Mpya,kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania leo imezindua huduma mpya ya kufanya malipo kwa njia ya kielektroniki.

001.VINJARI
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia(katikati)akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Vinjari na M PESA itakayowawezesha wateja wa mtandao huo kufanya malipo ya huduma katika sekta ya usafiri wa anga,mahoteli na utalii kwa njia ya kieletroniki huduma hiyo inapatikana kupitia tovuti ya vinjari,Wengine katika picha maafisa waandamizi wa tovuti ya vinjari kushoto ni Manase Banduka Mkurugenzi wa Uendeshaji,kulia Mkurugenzi Mtendaji Andrew Mboma

Huduma hii mpya inayozinduliwa leo inajulikana kama Vinjari na M-Pesa ambayo itawawezesha wateja wa Vodacom kufanya malipo ya huduma katika sekta ya usafiri wa ndege na utalii kwa njia ya kieletroniki kama ambavyo yamekuwa yakifanyika kwa kutumia kadi mbalimbali za kufanyia malipo kimataifa.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hii Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia amesema huduma hii kwa kuanzia itafanyika kwa kushirikiana na mtandao wa malipo ya kieletronikali nchini ujulikanao kama Vinjari.co.tz ambao unafanya kazi na zaidi ya taasisi 300 za kutoa huduma yakiwemo mahoteli ya utalii na makampuni mbalimbali yanayotoa huduma hususani za masuala ya utalii na sehemu za mapumziko na burudani.

002.VINJARI
Mkurugenzi Mtendaji wa tovuti ya Vinjari Andrew Mboma(kulia)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Vinjari na M PESA itakayowawezesha wateja wa Vodacom Tanzania kufanya malipo ya huduma katika sekta ya usafiri wa anga,mahoteli na utalii kwa njia ya kieletroniki huduma hiyo inapatikana kupitia tovuti ya vinjari

“Kadri siku zinavyozidi kusonga mbele tunazidi kushuhudia mapinduzi makubwa ya kiteknolojia hususani katika masuala ya biashara, Vodacom tumeona umuhimu wa kuanzisha huduma hii ili kuwawezesha wateja wetu kufanya miamala yao kwa njia ya kieletroniki kupitia huduma ya M-Pesa ili kwenda na wakati zaidi. Kwa kuanzia tutatoa huduma hii kupitia mtandao mpana wa malipo ya kielektronoki wa vinjari.co.tz na kadri siku zitakavyosonga mbele tutazidi kuboresha huduma hii,” alisema.

Aliongeza kuwa Vodacom inaelewa kuwa idadi kubwa ya Watanzania hawana kadi za kimataifa za kufanya miamala ya malipo kwa njia ya kielekroniki ndio maana imekuja na huduma hii ikiwa inawalenga wateja wetu wanaotumia huduma ya M-Pesa.

Naye Mkurugenzi wa Vinjari.com,Andrew Mboma amesema ili kupata huduma hii mteja anaingia katika sehemu ya kawaida ya kufanya miamala ya M-Pesa kwenye simu yake atakuta sehemu inayomuelekeza jinsi ya kupata huduma kupitia Vinjari na M-Pesa ambapo ataweza kufanya muamala kwa kadri ya huduma atakayokuwa anahitaji na atakatwa fedha kutoka akaunti yake ya M-Pesa kulipia huduma hiyo na malipo kidogo ya kutumia huduma hiyo. Maelezo zaidi yanapatikana kwa kutembelea tovuti ya vinjari.co.tz.

003.VINJARI
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia(kushoto)akipongezana na maafisa waandamizi wa tovuti ya vinjari (katikati ) Manase Banduka Mkurugenzi wa Uendeshaji,(kulia )Mkurugenzi Mtendaji wa tovuti hiyo Andrew Mboma wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Vinjari na M PESA itakayowawezesha wateja wa Vodacom kufanya malipo ya huduma katika sekta ya usafiri wa anga,mahoteli na utalii kwa njia ya kieletroniki huduma hiyo inapatikana kupitia tovuti hiyo

Katika miaka ya karibuni kumekuwepo na ongezeko kubwa la matumizi ya simu za mkononi nchini ambapo pia kumekuwemo na ongezeko la watumiaji wa mtandao wa internet.
Inakadiriwa kuwa zaidi ya watanzania milioni 28 wanatumia huduma za simu za mkononi ambapo zaidi ya watanzania milioni 6 wanatumia huduma za internet.
Mwisho

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents