Michezo

Picha/Video: Ndege iliyobeba wachezaji wa Brazil yaanguka Colombia

Ndege iliyokuwa imebeba watu 72, ikiwemo timu ya soka ya klabu ya Chapecoense ya Brazil, imeanguka katika sehemu ya milima nchini Colombia wakati inakaribia Mji wa Medellin.
cyz6pd7wgaa_jtw
Kabla ya kuanza safari timu hiyo ilipiga selfie hii.

Maelezo kamili ya ajali hiyo hayajafahamika lakini habari zinasema kwamba kuna watu 5 walionusurika.

Ndege hiyo ya kukodisha iliyokuwa ikitokea Bolivia, ilikuwa na timu ya soka ambayo ilikuwa icheze katika fainali ya Kombe la Amerika ya Kusini dhidi ya timu ya Atletico Nacional ya Medellin. Hivyo, fainali hiyo imeahirishwa.

583d17c2c36188d7598b4599

Ripoti zinasema ndege hiyo yenye leseni namba CP 2933, iliyoanguka muda mfupi kabla ya saa sita usiku, ilielezewa na Meya wa Medellin, Federico Gutierrez, kama “janga kubwa”, akiongeza kwamba inawezekana kuna watu walionusurika.

Angalia video ya wachezaji hao kabla hawajaondoka uwanja wa ndege.
https://youtu.be/CAgL8TmyU3M

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents