Habari

Prof Ndalichako awataka wazazi kuheshimu maamuzi ya walimu watoto wanapokosea

Serikali imewataka walimu kuwapa adhabu wanafunzi kulingana na mwongozo uliotolewa na serikali katika waraka wa adhabu wa mwaka 2002 huku akiwaasa wazazi kutowatetea watoto wao pindi wanapokosa nidhamu mashuleni.

ndalichako

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, alisema hayo Jumanne hii alipofungua mjadala wa wanafunzi kuelekea maadhimisho ya siku ya Haki za Binadamu, uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Waziri Ndalichako amesema kuwa wazazi wamekuwa wakiwavunja nguvu walimu kwa kuwatetea watoto wao hata kama wamekosa hivyo wanapaswa kuwa makini katika hili.

“Sasa hivi tumekuwa na changamoto ambazo unakuta wazazi wengine wanapenda kutetea watoto wao pindi wanapokuwa wanajiingiza katika utovu wa nidhamu,sasa hali kama hiyo inakuwa inawavunja nguvu walimu kwasababu unakuta bodi za shule hazifanyi kazi zao vizuri wazazi wanakuwa zaidi upande wa watoto wao kuwatetea hata pale ambapo inapaswa kukemea,” alisema Ndalichako.

Aidha waziri huyo ameendelea kuwasihi wazazi kushirikiana kwa karibu na walimu watoto wanapokuwa wakipewa adhabu na kuacha tabia ya kurudi upande wa watoto wao na kuwatetea.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents