Burudani

Q Boy Msafi adai kuambiwa hawezi muziki kunamtia hasira

Msanii wa Bongo Flava, Q Boy Msafi amesema kitendo cha kuambiwa hawezi muziki kunamfanya ajitume zaidi.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Unaanzaje’ ameiambia E-Newz ya EATV kuwa maneno ya namna hiyo yanamfanya kuongeza juhudi katika kazi, ila ni vitu ambavyo vipo kila mahali.

Mimi nachukulia kama changamoto kwa sababu ujue unapokuwa unasaka tonge lazima ukutane na changamoto za kukukatisha tamaa, kwa hiyo unapopata feedback kama hizo zinakufanya uongeze hasira na juhudi ili uweze kuprove wrong watu na vile ambavyo wanakufikiria,” amesema Q Boy.

Hata hivyo ameongeza kuwa mtu pekee anayeweza kusema hawezi kuimba ni producer na kueleza kuwa maproducer wote aliokwishafanya nao kazi akiwemo Mr. T Touch wanakubali uwezo wake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents