Recho: Nyimbo zangu nyingi huwa naandikia studio
Recho Kizunguzungu amesema hana desturi ya kuandika nyimbo zake kabla ya kuingia studio. Amesema nyimbo nzuri huziandika anapopata mzuka kutoka kwa producer.
“Kiukweli nyimbo zangu nyingi huwa siandiki yaani huwa inatokea studio hapo hapo, huwa napenda kuingia studio na kuanza kufanya kazi. Muziki ujue ni mood mtu hawezi akakuamsha asubuhi akakuambia uende studio, na usifanye kitu chochote ukiwa hauna mzuka huwezi kufanya kitu” Recho aliiambia Bomba FM ya Mbeya.
Kwa upande mwingine Recho alisema kujitambua kwake ndio njia kuu inayomfanya asiteteleke katika muziki kutokana na kuutegemea zaidi katika kupata kipato cha kuendeshea maisha yake. “Siri kubwa nikujua ni kitu gani unakifanya, kwa sababu kuna mtu mwingine anakuwa anafanya halafu hajui kitu gani anakifanya, yaani hajielewi yuko wapi? Mimi ninafanya muziki halafu muziki ndio maisha yangu.”