Michezo

Rio Ferdinand: Sancho ameonyesha Ten Hag ni mtu gani

Staa wa Soka wa Klabu ya Manchester United Rio Ferdinand ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa vipindi vya michezo amesema kuwa aliyekuwa winga wa Manchester United ambaye kwasasa anakiwasha vilivyo Borrusia Dortmund Jodan Sancho ameonyesha wazi kile kinachodhaniwa na watu kuhusu uwezo mdogo wa kocha wa Manchester United kuhusiana na mahusiano na wachezaji.

“Sancho kama ilivyokuwa kwa Ronaldo na wengine anaendelea kutuonyesha kuwa Ten Hag ana walakini kwenye namna ya kuhusiana na wachezaji”.

“Kuna namna ya kutatua mapungufu ya wachezaji na siyo kutaja kama vile kwenye vyombo vya habari wachezaji wote walioondoka kwa mgogoro na yeye hivi sasa wanafanya vyema kuliko timu yake” alisema Rio.

Rio anasema hayo baada ya kiwango bora cha sasa cha Sancho ambaye ameisaidia Dortmund kufuzu nusu fainali ya Uefa akilinganisha na mafanikio ya Ronaldo baada ya kuondoka United huku United chini ya Ten Hag ikiwa kwenye hali mbaya zaidi.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents