Michezo

Gamondi apiga Mkwara Kambini Yanga SC

Yanga imeingia kambini jana tayari kwa maandalizi yao ya kuwakaribisha watani wao Simba, lakini kuna mkwara mzito wameshushiwa mastaa wao kisa Wekundu wa Msimbazi.

Yanga itakuwa mwenyeji wa Simba, Jumamosi April 2024 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa Uwanja wa Benjamini Mkapa  Dar es Salaam mechi ambayo kwa namna yoyote inakuwa na presha kubwa ndani na nje ya Uwanja. Simba wao wamejificha Zanzibar.

Wakati Yanga ikiingia kambini jana, mastaa wake wakakutana na mkwara mzito kwenye kikao kwenye kikao dhidi ya viongozi wao wa juu, waliwaambia hawatakiwi kabisa kuchukua makelele ya mashabiki kuwa watani wao kikosi chao ni dhaifu na kinafungika kirahisi.

Kikao hicho kilichofanyika kambini kikiongozwa na Rais wa klabu hiyo Eng. Hersi na hata kocha wao Miguel Gamondi alikazia. Habari zinasema katika kikao hicho cha siri wachezaji waliambiwa wanatakiwa kujiandaa na Dakika 90 ngumu mbele ya watani wao ambazo huenda zikawa na Sapraizi kuliko wanavyodhania hivyo wasiende na upepo wa Kishabiki.

“Tumewaambia kwamba wanatakiwa kuachana na makelele ya mashabiki, kwani wachezaji kazi yao ni kwenda kuutafuta ushindi kwa kucheza bila dharau na kuipigania timu uwanjani kwa umakini mkubwa wakati mashabiki kazi yao ni kupiga kelele majukwaani, ‘”Alidokeza bosi mmoja aliyekuwa kwenye kikao hicho kilichotoka na mkakati kwamba Jumamosi ni fainali ya Ubingwa wao.

Mapema Kocha Gamondi alisema hawawezi kuwa na akili za mashabiki wao kwa kuona kama mchezo huo ni rahisi na kwamba wataifunga Simba kirahisi.

“Sisi sio mashabiki, sisi ni Profrshno hatuwezi kufanya makosa hayo tumeshinda mechi hizi zote kwa kutanguliza weledi kwa kuwaheshimu kwanza wapinzani wetu bila kujali changamoto zote” Alisema Gamondi.

“Tunauhitaji ushindi huu kama ambavyo tumekuwa tukihitaji kushinda mechi zilizopita, tutakwenda kucheza mechi hii bila presha kwa kutumia Falsafa yetu kuweza kushinda mechi hii na haitakuwa rahisi kabisa”.

Hii inakuwa ni mechi ya tatu kwa Gamondi dhidi ya Simba msimu huu ukiwa wa Kwanza kwake akiwa Yanga, alikutana na Wekundu wa Msimbazi katika Ngao ya Jamii akapoteza kwa penati kisha akaja kushinda 5-1 ndani ya ligi wakati timu hiyo ikiwa chini ya Kocha Roberto Oliveira “Robertinho”.Hivi saa anakwenda kukutana na Simba ikiwa inaongozwa na Abdelhak Benchikha.

 

 

 

 

 

cc:Tanzaniaweb.Live

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents