Habari

Taarifa mpya ya TMA kuhusu hali mbaya ya Hewa

Mamlaka ya Hali ya Hewa  Tanzania (TMA) imetoa taarifa ya matarajio ya hali ya hewa kwa siku tano kuanzia saa 9:30 mchana Jumanne April 16, 2024.

TMA imetoa tahadhari ya upepo mkali unaozidi Kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayozidi mita mbili kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi.

Maeneo hayo ni ya mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani (Ikijumuisha na Visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Mamlaka hiyo imesema uwezekano wa kutokea kwa hali hiyo ni mkubwa na kiwango cha athari zinazoweza kutokea ni wastani.

TMA pia imetoa angalizo la Mvua kubwa kwa maeneo machache ya mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani (Ikijumuisha Visiwa vya Mafia) na visiwa vya Unguja na Pemba.

Mamlaka hiyo imesema uwezekano wa kutokea ni wastani na kiwango cha athari zinazoweza kutokea ni wastani.

Athari zinazoweza kujitokeza kwa mujibu wa TMA ni mafuriko, kuathirika kwa baadhi ya maeneo na shughuli za kiuchumi, uvuvi na usafirishaji baharini, ikiwataka wahusika kuchukua hatua.

April 17, 2024

Mamlaka imetoa angalizo la mvua kubwa kwa maeneo machache ya mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Tanga, Pwani (Ikijumuishwa visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara na Visiwa vya Unguja na Pemba.

Pia imetoa angalizo la upepo mkali unaofikia Kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita mbili kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi (mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya mafia) Lindi na Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

TMA imesema uwezekano wa kutokea ni wastani na kiwango cha zinazoweza kutokea pia ni wastani.

Athari hizo kwa Mujibu wa TMA ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji na kuathirika kwa baaadhi ya shughuli  za kiuchumi, Uvuvi na usafirishaji baharini.

 

April 18, 2024

TMA imetoa angalizo la mvua kubwa kwa maeneo machache ya mikoa ya Dar es Salaam, Pwani (Ikijumuishwa na visiwa vya Mafia) , Lindi na Mtwara pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba.

Taarifa ya TMA imesema uwezekano wa kutokea hali hiyo ni wastani na kiwango cha athari zinazoweza kutokea pia ni wastani.

Athari hizo kwa mujibu wa TMA ni baadhi ya Makazi kuzungukwa na maji, pamoja na kuathirika kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi, uvuvi na usafirishaji baharini, ikitaka angalizo hilo kuzingatiwa..

 

April 20, 2024

TMA imetoa angalizo la mvua kubwa kwa maeneo machache ya Mkoa wa Tanga na Visiwa vya Unguja na Pemba.

Pia imetoa angalizo la upepo mkali kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofika mita mbili kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi (Mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (Ikijumuisha visiwa vya Mafia ) Lindi na Mtwara pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba.

Mamlaka imesema uwezekano wa hali hiyo kutokea ni wastani na kiwango cha athari zinazoweza kutokea ni wastani.

TMA imesema athari zinazoweza kujitokeza ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji, pamoja na kuathirika kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi, uvuvi na usafirishaji baharini.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

CC:Tanzaniaweb.Live

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents