Technology

Sahau kuhusu password, sasa utatumia sura yako kuingia Facebook

Mtandao wa Facebook upo mbioni kufungua huduma ya ‘facial recognition’ ambapo watumiaji wa mtandao huo watatumia sura zao kama utambulisho wa kuingia kwenye mtandao huo.

Ujio huo umekuja baada ya Facebook kupata malalamiko ya matatizo mengi ya watumiaji wake kusahau nywira (Password) au email (Barua pepe) za kuingilia kwenye mtandao huo maarufu zaidi duniani.

Hatua ya Facebook inakuja baada ya kampuni ya Apple Inc kuzindua huduma ya utambuzi wa sura (Apple Face ID) kwenye ulinzi wa simu yake ya iPhone X.

Huduma hiyo ya utambulisho wa sura kwa watumiaji wa facebook, itafanya kazi baada ya mteja kusijasili kwa njia ya kawaida na baadae ataanza kutumia njia hiyo ya kisasa.

Katika matumizi mteja wa facebook ataweka simu yake mbele ya sura yake na kuanza kurekodi sura yake kwa kuitazama kamera na baadae ataletewa ujumbe wa kutambuliwa (Verified) kutoka facebook.

Tupo kwenye majaribio kuona ni jinsi gani wateja wetu wanaweza kuingia haraka kwenye akaunti zao bila wasi wasi wa kusahau password na utambulisho huo tunatarajia kuuweka kwa mfumo wa sura zao,“amesema msemaji mkuu wa Facebook kupitia mtandao wa habari za teknolojia wa Tech Crunch.

Kwa sasa kama umesahau namba za siri za akaunti yako mtandao wa facebook unatumia picha za marafiki zako ili uweze kuzitambua na baadae kurudisha akaunti yako.

Hata hivyo huduma hii tutarajie kuipata mwishoni mwa mwaka huu au mwanzoni mwakani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents