Habari

Serikali yaridhika na Sanamu ya Nyerere iliyopo Ethiopia

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa amesema kuwa serikali imeridhika na sanamu ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere iliyopo Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) Addis Ababa, Ethiopia.

Balozi Mussa ameyasema hay oleo Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akijibu swali yaliyoulizwa wakati wa mkutano wa wahariri wa vyombo mbalimbali vya Habari nchini kuhusu ziara alizofanya Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Amesema serikali imefuata maelezo ya kitaalamu ambayo yalitolewa na Kamati maalum ya wataalamu kuhusu sanamu hiyo ambayo imeridhia sanamu hiyo.

Mussa amesema wajumbe wa Kamati hiyo walitoka maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na familia ya Nyerere, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na Wizara ya Mambo ya Utamaduni, Sanaa na Michezo

Amesisitiza kuwa Mwalimu Nyerere anayeonekana kwenye sanamu ni yule wa miaka 1960 na 1980 na kwamba taratibu za kitaalamu zinaeleza kuwa ili sanamu ithibitishwe ni ya mtu fulani ni lazima mfanano wake ufikie asilimia 75 na kwa upande wa sanamu hiyo mfanano wake ulifikia asilimia 92.

“Kweli kumekuwa na mtazamo tofauti wapo waliosema kuna itilafu, ila upande mwingine wanakubali na kusema kwamba ni Mwalimu Nyerere, Serikali katika hili imefuata maelezo ya kitaalamu kutoka kwenye kamati ambayo iliridhika kabisa na sanamu hiyo.

“Mwalimu anayeonekana katika sanamu hiyo ni yule wa miaka 1960 hadi 1980 pili kauli ya mtoto Madaraka Nyerere amesisitiza kwamba yule ni baba yake nak ama kuna mtu anayebisha basi amuulize yeye,” amesema Balozi Mussa

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents