Habari

Serikali yatoa taarifa kuzama kwa kivuko cha Kilombero

Serikali imetolea ufafanuzi kuhusu ajali ya kuzama kwa Kivuko cha mto Kilombero mkoani Morogoro kikiwa na abiria zaidi ya 30 na magari yapatayo watatu.
jeni

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Bungeni Dodoma na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama alisema mpaka sasa tayari watu 30 wameshaokolewa.

“Kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwa masikitiko makubwa naomba nitoe taarifa ya awali kuhusiana na taarifa ambayo Mh Naibu spika umehitoa hapa na umesema meza yako umeipata. Mh Naibu spika serikali imepokea taarifa usiku wa jana kuamkia leo, kwamba kivuko cha Kilombero kimepata ajali na kuzama. Kwa maelezo ya awali Mh Naibu spika kulikuwa na abiria 31 ambapo abiria 30 walisha okolewa, hata hivyo kivuko hicho kilikuwa na magari matatu na bajaji mbili kwa taarifa za awali. Hali ya mawasiliano ya barabara kupitia kivuko hicho yamekatika na kuacha kutokuwepo kwa mawasiliano kati ya Kilombero na Wilaya na Ulanga. Mh Naibu spika naomba niwaambie watanzania jitihada za wokozi zilianza toka jana, katika maafa hayo yaliyotokea ili kuhakikisha kwamba abiria na mali, na hasa maisha ya abiria yanaokolewa kwa haraka. Kamati zote za usalama katika ngazi ya Wilaya na Mkoa vile vile taasisi za maafa zinazoshughulika na maswala ya mahafa katika ngazi za Mkoa, zimeendelea kushughulikia swala hilo kwa nguvu zote. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano aliondoka toka jana usiku kwa agizo la Mh Waziri Mkuu kuelekea kwenye eneo la tukio kwa kazi maalum ya kwenda kufanya usimamizi wa uongozi wa uokoaji katika eneo la tukio. Mh Naibu spika timu za utendaji za serikali ziko kazini katika kushughulikia tatizo hilo la maafa, lakini hasa pia kuona ni namna gani tunaweza kurudisha mawasiliano ya Wilaya hizo mbili, hii ni pamoja na kulishirikisha jeshi letu la wananchi wa Tanzania kuona wanaweza kutoa msaada gani wa haraka ili pande hizo mbili zirudishe mawasiliano kwa haraka. Nawaomba watanzania watulie serikali toka ilipo pokea taarifa hiyo jana imekuwa ikifanya kazi kubwa yakuona nini kifanyike kwa wakati gani ili kuweza kutatua tatizo la janga na maafa hayo yaliyotokea,” alisema Jenista Mhagama

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents