Habari

Serikali yavunja rekodi ukusanyaji mapato kwa mwaka mpya wa fedha wa 2017/18

Serikali ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Mapato (TRA) imevunja rekodi katika ukusanyaji wa mapato kwa miezi tisa ya mwaka mpya wa fedha wa 2017/18 kuanzia Julai, 2017 hadi Machi, 2018 .

Tokeo la picha la Richard Kayombo
Richard Kayombo

Taarifa iliyotolewa leo Jumanne Aprili 10, 2018 na Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi (TRA), Richard Kayombo imeonesha kuwa serikali kwa miezi tisa imekusanya kiasi cha tsh Trilioni 11.78 likiwa ni ongezeko la ukuaji kwa asilimia 8.46%, ukilinganisha na mapato yaliyokusanywa kwa mwaka wa fedha uliopita wa 2016/17 ambapo serikali ilikusanya kiasi cha Tsh Trilioni 10.86 .

Bwana Kayombo amesema kuwa mafanikio hayo ya ongezeko la kodi yametokana na elimu iliyotolewa kwa Wananchi juu ya ulipaji kodi na uzalendo kwa watendaji kazi wake kumechangia kufikia makusanyo hayo.

Soma taarifa zaidi;

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents