Burudani

Shilole: Niliona nichanganye location za nyumbani na Ubelgiji ili kuongeza ubora wa video ya ‘Melele’

Shilole alikuwa na deni kwa mashabiki wake ambao walikuwa wakisubiri video ya ‘Malele’, ambayo hapo awali alisema imeshutiwa location tatu tofauti za Brussels, Amsterdam na uholanzi (Ingia hapa).

https://youtu.be/rr5-InrpBMQ

Baada ya video ya ‘Malele’ kutoka imeonekana imeongozwa na director wa Tanzania, Khalfani na ina mchanganyiko wa location za Tanzania na clip chache za nje.

Shilole ameiambia Bongo5 sababu za kuamua kurudia kushoot Tanzania na kuchanganya na clip chache za location za Ubelgiji.

“Kama ulivyoweza kuitazama video vizuri kuna clip za Ubelgiji ambazo zipo mule, kwahiyo niliona kwamba ili niweze kufanya vizuri zaidi lazima nishoot na hapa nyumbani, ili kuongeza ubora zaidi kwasababu kule Ubelgiji sikuwa na dancers wala nini, kwahiyo hapa umeweza kuona nime dance na dancers na tukaongeza baadhi ya location na baadhi ya clips za Ubelgiji zipo, nadhani video ni nzuri imeleta ladha tofauti nimeweza kuweka nyumbani na Belgium.” Alisema Shishi baby.

Shilole ameongeza kuwa licha ya kutumia location zaidi ya moja alipokuwa Ubelgiji, lakini hazikuweza kutumika kwenye video kwasababu director Khalfani alisema hazikutoka vizuri.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents