Michezo

Simba haponi kama binadamu – Ibrahimovic

Baba mwenye nyumba huyo anakuja. Zlatan Ibrahimovic amewashtua watu kutokana na hali yake ya afya inavyozidi kuimarika haraka tofauti na ilivyotangazwa hapo mwanzo.

Mchezaji huyo alitajwa kuonekana tena uwanjani mwakani baada ya kuumia mguu wake wa kulia katika mechi yao robo fainali ya kombe la Europa League dhidi ya Anderlecht na kufanyiwa upasuaji, lakini hali imekuwa tofauti baada ya kuonekana kuanza mazoezi madogo madogo na kutarajiwa kuwa fiti mapema mwanzoni mwa msimu huu.

Katika kuonyesha hali yake inaendelea vizuri, Ibrahimovic ameweka video katika mtandao wa Instagram ikimuonyesha akifanya mazoezi ya kupiga mpira na kuandika, “The touch will never disappear. Lions dont recover like humans.”


Zlatan akiwa chini akiugulia maumivu wakati wa mechi yao dhidi ya Anderlecht

Zlatan ameifungia Man United magoli takribani 28 tangu ajiunge na timu hiyo msimu uliopita akitokea PSG kama mchezaji huru.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents