Michezo

Simba wasubiri pointi 3 za CAF

Klabu ya Simba imetoa taarifa kuwa imepeleka barua rasmi kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuomba uchunguzi kuhusu Klabu ya Al-Merreikh ya Sudan kuwachezesha wachezaji wawili waliofungiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Sudan katika mchezo namba 93 wa Klabu Bingwa ya Afrika dhidi ya Simba uliyopigwa Machi 6, mwaka huu mjini Khartoum nchini humo.

Wachezaji hao ni Ramadan Ajab na Bakhiet Khamis ambao walifungiwa kutojihusishwa na michezo kwa miezi sita kuanzia Januari 21, 2021 kutokana na kila mmoja kua na mikataba na timu mbili tofauti.

Mabingwa hao wa nchi wanasubiria kupokea taarifa za uchunguzi kutoka CAF juu ya jambo hilo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents