Burudani

Stamina kumbembeleza mpenzi wake na ‘Love Me’

Msanii wa muziki wa hip hop kutoka Morogoro, Stamina ‘Shorwebwenzi’ anarudi upya kivingine kwa kuachia wimbo wake ‘Love Me’ ambao ni maalum kwa wapendanao.

Rapa huyo ambaye amezoeleka kwa ngoma za harakati na michano mikali, safari hii ameamua kulegeza kidogo kwa kuandaa wimbo wa mapenzi akiwa na Maua Sama.

“Kama nilivyosema awali mashabiki wangu mtarajie Stamina mwingine, Stamina mkali, ngoma ya utofauti kama ulivyosikia ujio wa ‘Love Me’ nikiwa na Maua Sama,” Stamina aliimbia Bongo5 “Kwahiyo mashabiki wangu wasubirie ‘Love Me’ ni ngoma kali na ina maneno kumtu ya mapenzi, utaona namna wapenzi wanavyozungumza,”

Aliongeza, “Audio itatoka alhamisi hii lakini pia video iko tayari itatoka Ijumaa. Kwahiyo sina mengi ya kusema zaidi ya kuwataka mashabiki wangu waisubirie ngoma kwa hamu kwasababu ni ngoma  kali,”

Pia rapa huyo amedai kwa sasa anafanya kazi chini ya record label ambayo hakutaka kuiweka wazi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents