Bongo Movie

T-Junction yanyakuwa tuzo kubwa za filamu nchi Kenya

Filamu ta T-Junction iliyoandaliwa chini ya Kijiweni Production inazidi kuleta matumaini mapya katika sekta ya filamu nchini kwa kuendelea kuzoa tuzo za mbalimbali filamu nje ya nchi.

Kupitia filamu hiyo mwanadada Magdalena Christopher amefanikiwa kujakua tuzo ya ‘Udada International Women’s Film Festival’ ya nchini Kenya, kupitia kipengere cha’ Best Actress’

Naye Lester Milado kutoka katika filamu hiyo hiyo ya TJuction ameweza kunyakuwa tuzo ya ‘Best Cinematography’ kwa mwaka 2017.

Miezi michache nyuma filamu hii inayoelezea maisha halisi ya kiTanzania ilifanikiwa kunyakua tuzo kadhaa za Zanzibar Films Festival (Ziff) ikiwemo ya muigizaji bora wa kike na iliyoenda kwa mwanadada Hawa, pia kutoka nje katika tuzo za Zimbabwe International Films Festival(ZIFF) kwa ushirikiano na International Image Films Festival(IIFW) kupitia kipengele cha Best Africa at Women International Films Festival.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents