Burudani

TID asema anajipanga kuweka kambi Kenya ili kutanua wigo wa muziki wake

Msanii wa muziki TID amefunguka kwa kusema kuwa, anajipanga kuweka kambi nchini Kenya baada ya kugundua muziki wake una soko kubwa nchini humo.

TID 1

Akizungumza na bongo5 leo, TID amesema kuwa amekuwa akipata feedback ya muziki wake kutoka Kenya, huku akidai kuwa wimbo wa ‘Presha’ aliofanya na Nazizi unashika chati mbalimbali za radio.

“Sasa hivi siwezi kuzungumzia project yoyote kwa sababu kuna kazi ambayo ina mwezi mmoja, inaitaji nguvu nyingi sana kui-support, hapa Tanzania inaenda slow lakini inaenda vizuri, ila Kenya inaenda vizuri sana, jana nilikuwa na ongea na Willy Tuva wa Kenya anasema kule wimbo unafanya vizuri sana na umeshika chati mbambali za TV, mimi Kenya na soko kubwa sana la muziki wangu na hivi ninavyokwambia mwezi ujao nataka niweke Kambi kule, kwajili ya show, promotion za kazi zangu, sijajua itakuwa muda gani kwa sababu sasa hivi ndo nipo kwenye maandalizi,” alisema TID.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents