Michezo

Tumekaa na baba yake Chama, nimemualika – CEO wa Simba Barbara akiwa Zambia

CEO wa Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba SC, Barbara Gonzalez amesema kuwa wamekaa pamoja na baba mzazi wa Clatous Chama hapo jana baada ya kumualika kwenye mchezo wao dhidi ya Red Arrows ya Zambia.

Kuangalia video bofya HAPA

”Leo tumekaa na baba yake Chama, nimemualika, unajua ukiwa umesajiliwa Simba SC hata ukiondoka unaondoka kwa wema, hivyo leo nimekaa na baba yake Chama tumemualika hapa uwanjani amefurahia mechi, tumekaanaye asubuhi kwenye kifungua kinywa, bado sisi ni familia.”

Kumekuwa na tetesi kuwa nyota huyo anarejea nchini lakini kitendawili ni je atatua Simba ama kwa watani wao Yanga hakijapatiwa majibu baada ya kundoka Msimbazi msimu uliyopita kwa kuuzwa kwa dau nono kwelikweli la Bilioni 1.5 kwenda RS Berkane FC ya Morocco.

Katika mchezo huo wa hapo jana Simba ilifungwa goli 2 – 1 dhidi ya Red Arrows, hata hivyo imepata nafasi ya kusonga mbele katika hatua ya makundi kwa aggreget ya 4 – 2 baada ya ushindi wa 3 – 0 waliyopata kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Benjamin Mkapa.

Imeandikwa na @fumo255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents