Burudani

Tunasubiri Lady Jaydee atakavyoinuka tena

Nimekuwa shabiki wa Lady Jaydee toka way back! Nakumbuka nilianza kumsikiliza nikiwa kidato cha nne. Machozi ndiyo ulikuwa wimbo ulionitambulisha kwenye ulimwengu wa malkia huyu wa Bongo Flava na kuniteka kwenye himaya ya muziki wake.

12798131_967611659983004_635376460_n
Kutoka kushoto: Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dr Charles Kimei, Seven Mosha na Lady Jaydee

Sikuishia tu kusikiliza wimbo huo bali pia album yake ya kwanza iliyokuwa na jina hilo hilo. Hii hadi leo naichukulia kama moja ya album za dhahabu zilizotolewa Tanzania.

Jide aliendelea na mwendo wake wa kuachia kitu baada ya kitu na hadi sasa huenda ndiye msanii wa Bongo Flava mwenye santuri nyingi zaidi. Machozi ilifuatiwa na Binti (2003), Moto (2005), Shukrani (2007), Ya 5. The Best of Lady Jaydee (2012) na Nothing But The Truth (2013).

Fast forward.. Mara ya mwisho kumsikia Jide ni kwenye Give Me Love aliyofanya na Uhuru na Mazet wa Afrika Kusini. Baada ya hapo amekaa kimya hadi leo. Kuna wakati nilianza kuhisi kuwa huenda Jaydee ameamua kupumzika kimoja kwasababu ukimya wake ulikuwa wa kutisha.

Lakini kama wasemavyo wahenga, kimya kingi kina mshindo mkuu. Miezi kadhaa iliyopita, Jaydee aliongeza nguvu kwenye management yake kwa kumfanya Seven Mosha kuwa meneja wake. Jaydee na Seven ni marafiki wakubwa na wamefahamiana kwa miaka mingi sana.

12407708_1674985029384341_649714702_n
Mwaka 2000: Lady Jayde akiwa na Taji Liundi na Seven Mosha

CV ya Seven Mosha si haba. Maisha yake mengi yamekuwa kwenye tasnia ya burudani na tena akifanya kazi kwenye makampuni ya kimataifa. Amewahi kufanya kazi na MTV, Sony Music Africa na makampuni mengine. Kwa sasa pamoja na kuwa na Laydee kama meneja wake wa kibiashara, anafanya kazi na Alikiba, Navaa Grey na Philip Nwankwo.

1172219_160953367603974_1540394864_n
Seven na Lady Jaydee

Back to Lady Jaydee. Hivi karibuni ameanzisha kampeni ya siku 30 kutuandaa kuja na mradi wake mpya, ‘Naamka Tena.’ Mradi huu tumeona ukipewa mashavu na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa kisiasa.

Hadi sasa walioonekana kumpa shavu Jide ni pamoja na Waziri wa Ardhi William Lukuvi, Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dr Charles Kimei, Meneja Udhamini wa TBL, George Kavishe, Miss Tanzania wa zamani, Millen Magese na wengine kibao.

Naamka Tena ni nini?

Well, bado sijapata jibu la moja kwa moja na hata kama nikisema nimuulize Jide, hawezi kusema kwasababu ataondoa ile excitement anayoijenga kwa siku 30. Na kiukweli ni bora tuendelee kusubiri hizo siku ziishe ile surprise iweze kuwa kubwa zaidi.

Lakini kitu kilichowazi ni kuwa ‘Naamka Tena’ inaweza kuwa ni jina la album yake mpya. Nachelea kusema kuwa ni single tu kwasababu kwa ninavyomjua Lady Jaydee, hawezi kutease kitu kwa mwezi mzima na kisha kuachia tu single moja. Hata ikiwa ni single tu, ni habari njema kwa mashabiki wake na wapenzi wa muziki wa Tanzania.

Chochote anachotuletea, tunaamini kitakuwa ni kitu kikubwa hasa kwakuwa katika ukimya wake, amekuwa akisafiri na kukutana na wasani wengi wakiwemo wa Kenya na hivyo bila shaka amekuwa na muda wa kutosha kuandaa santuri mpya.

Zimebakia siku 15 tu hadi Jaydee atakapoamka tena.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents